Wanaotupa taka ovyo Mombasa kulipa faini ya elfu 50 au kufungwa

January 10, 2018

Wizara ya Mazingira  kaunti ya Mombasa imetishia kufunga baadhi ya maeneo yasiostahili kuwa jaa la taka katika kaunti hiyo.

Kwenye mkao na Wanahabari mjini Mombasa, Waziri wa Mazingira katika serikali ya kaunti hiyo Godfrey Nyongesa amesema kuwa tayari serikali ya kaunti hiyo imefanikiwa kufunga baadhi ya sehemu sizisostahili kuwa jaa la taka.

Nyongesa amehoji kuwa hatua hiyo itasaidia kudhibiti maradhi mbalimbali yaliyo hatari kwa wakaazi na yanayoshuhudiwa kwa sasa katika kaunti hiyo ya Mombasa.

Nyongesa pia amewaonya Wananchi wenye tabia ya kutupa taka ovyo, akisema kuwa atakayepatikana atapigwa faini ya shilingi elfu 50 ama atumikie kifungo cha miezi sita gerezani

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.