Wanasiasa walaumiwa kwa kuchipuka kwa magenge ya uhalifu

July 9, 2018

KECOSE

Shirika la kijamii la KECOSCE limeelekezea kidole cha lawama viongozi wa kisiasa kwa mchipuko wa magenge ya kihalifu yanayohangaisha wakaazi katika kaunti ya Mombasa na maeneo mengine nchini.

Kulingana na mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Phyllis Muema magenge ya wahalifu huongezeka msimu wa uchaguzi kwani   viongozi wa kisiasa huwatumia vibaya vijana kujiongezea umaarufu.

Akizungumza mjini Mombasa Bi Muema amefichua kwamba wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita shirika hilo lilipokea ripoti nyingi zinazohusisha baadhi ya viongozi wa kisiasa kufadhili makundi ya vijana kuzua vurugu.

 Mkurugenzi huyo aidha amedokeza kwamba magenge hayo ya kihalifu yamepungua kwa kiasi kikubwa baada ya msimu ya uchaguzi kukamilika   hali inayodhihirisha wazi kuwa huenda viongozi wa kisiasa hufadhili makundi hayo.

Taarifa na Cyrus Ngonyo.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.