Wanasiasa walaumiwa kwa ongezeko la masaibu miongoni mwa Vijana Mombasa

February 8, 2019

Mwanaharakati wa vijana katika eneo la Tononoka, kaunti ya Mombasa Abdulhamid Abdulrahman amesema wanasiasa katika kaunti hiyo wamechangia pakubwa katika masaibu yanayowakumba vijana wa Mombasa.

Kulingana na Abdulhamid, vijana wamekuwa watumwa wa wanasiasa kwa kutumika kutekeleza mambo yalio kinyume na maadili ya kijamii.

Abdulhamid amewataka viongozi wa kisiasa kukomesha hali hiyo na kuimarisha hali ya maisha ya vijana ili wajiondoe katika hali hiyo ya kutumiwa visivyo hasa nyakati siasa zinapochacha.

Wakati uo huo, Kiongozi huyo wa vijana amewataka vijana wenyewe kuwa na msimamo na kubadili hali yao ya maisha badala ya kukubali kuwa watumwa wa wanasiasa wa kaunti hiyo.

Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.