Wanawake ni wa kufunika na kubandua – Bin Kalama

June 28, 2018

Msanii anayepeta na mziki wa kitamaduni Bin Kalama ameshangaza wengi kwa kudai kuwa wanawake ni wa kutumiwa na kuachwa.

Bin Kalama aaliyevuma na kibao “Zawadi” wakati mmoja anasema kuwa safari yake katika mapenzi imemkutanisha na wanawake kumi na wote ameachana nao kwa sababu moja tu.

“Wanawake hawaamini wanamuziki, hata ukampenda vipi yeye atazua mpaka umwache. Hawa ni wa kubandika na kubandua tu,” amesema Bin Kalama.

Kwa sasa msanii huyo anajitayarisha kufunga ndoa yake ya kumi.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.