Wanoendeleza biashara ya Kamari waonywa 

November 24, 2018

Afisa mkuu wa bodi ya filamu nchini kanda ya Pwani Boniventure Kioko amewatahadharisha wakaazi wa maeneo ya mashinani wanaoendeleza biashara ya michezo ya kamari kwamba watakabiliwa.

Akiongea mjini Mombasa Kioko amesema kuwa wamiliki wengi wa mashini za mchezo wa kamari wamezihamisha sehemu za  mashinani kuendeleza biashara hio na kuwapotosha watoto wenye umri mdogo.

Kioko amesema kuwa wanapanga kufanya msako mkali wa kusaka na kusambaratisha mashini hizo akisema kuwa zimewafanya watoto wengi kuwa wezi  na kutozingatia masomo yao.

Hata hivyo amewataka wazazi kuwa karibu na watoto wao hususan kipindi hiki cha likizo ya mwisho wa mwaka ilikuona kwamba hawajihusishi na mambo yasiofaa.

Taarifa na Hussein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.