Wasanii wa Mombasa wamelala- Masauti

December 29, 2017

Msanii Mswazi Masauti amefunguka na kuelezea tatizo linalokumba wasanii kutoka ukanda wa Pwani.

Akizungumza na kituo kimoja cha radio humu nchini, Mswazi amesema kuwa wasanii wengi wa Pwani wamelala sababu inayowafanya kutopata faida.

“Wasaniiwa Mombasa wamerelax sana,” amesema Masauti.

Zidi ya hayo amefichua kuwa wengi wao hawapendi kuwekeza katika kazi yao hali inayozifanya kazi zao kukosa mvuto.

“Halafu hawataki ku upgrade kimziki tofauti ambao uko kwa soko kwa sasa. Halafu pia mtu anaona ugumu kuwekeza katika kazi yake,” amesema Masauti.

Taarifa na Dominick Mwambui.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.