Wasanii wa Pwani waunga mkono vita dhidi ya Mihadarati

June 21, 2018

ERIC OMONDI

Picha/Kwa hisani

Siku chache baada ya mchekeshaji Eric Omondi kufichua hali ya marehemu kakake kutokana na uraibu wa mihadarati, wasanii kutoka ukanda wa Pwani wameungana na kikosi cha Radio Kaya katika kampeni dhidi ya utumizi wa madawa ya kulevya.

Radio Kaya kwa ushirikiano na shirika la Samba Sports Youth Agenda imekuwa na kampeni ya kuwaasia watoto dhidi ya utumizi wa mihadarati kupitia mchezo wa soka.

Ni katika harakati hii ambapo wasanii Dogo Richy, Chikuzee na ABK na Shephard wamejiunga na kituo hicho.

17 08 17 DOGO

Msanii Dogo Richiy

Akizungumza na Uhondo Dogo Richy amefichua kuwa utumizi wa mihadarati umekuwa ukipoteza talanta nyingi ukanda wa Pwani nanisharti juhudi zichukuliwe ili kuokoa kizazi kichanga.

“Tumeona wasanii wengi wazuri wakipotea kwa sababu ya mihadarati, iwapo hatutaanza kuchukua hatua basi talanta zitakuwa zikipotea pasipokuwa na umuhimu katika jamii. Naunga mkono harakati hii ili kuonyesha jamii kuwa muda umefika sote tusimame dhidi ya mihadarati,”amesema Dogo Richy.

CHIKUZEE

Msanii Chikuzee

Kwa upande wake Chikuzee amewasisitizia wazazi kuwa katika mstari wa mbele wa kuwakinga watoto wao dhidi ya utumizi wa mihadarati.

“Kwa wazazi wengine ni wepesi kutumia vileo mbele ya wazazi wao. hili ni jambo ambalo hupelekea urahisi kwa watoto kuanza kuonja onja. kwa hivyo ni muhimu azazi wawe watu wa kwanza kuwakinga watoto,”amesema Chikuzee.

Taarifa na Dominick Mwambui.

 

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.