Washiriki wa Mchuano wa Spika Kilifi watafutwa

July 2, 2018

Mchuano wa kutafuta timu bora zitakazo shiriki katika kinyang’anyiro cha ligi ya Spika  wa bunge la kaunti ya Kilifi kimeng’oa nanga katika wadi ya Shimo la Tewa.

Spika wa bunge la kaunti hiyo Jimmy Kahindi amesema kuwa ligi hiyo inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni itajumuisha timu 35 kutoka wadi zote za za kaunti ya Kilifi huku ikiwa na nia ya kutambua na kukuza vipaji vya vijana.

Kwa upande wake Naibu Gavana wa kaunti hiyo, Gidion Saburi ameipongeza hatua hiyo na kuitaja kama chanzo cha kukabiliana na tabia potovu miongoni mwa vijana.

Wadi ya Shimo La tewa itwakilishwa na Mtwapa City chini ya ufadhili wa mwakilishi wadi hiyo Sammy Ndago. Timu hiyo imepata ufadhili wa kitita cha shilingi 50,000.

Taarifa na Marieta Anzazi.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.