Washukiwa 16 wanaodaiwa kuteketeza basi la kampuni ya Simba coach wakamatwa

January 8, 2018

Washukiwa 16 wanaodaiwa kuhusika kwenye kisa cha kuteketeza basi la Kampuni ya Simba Coach eneo la Kijiwe Tanga huko Malindi wanazuiliwa katika kituo cha Polisi cha Malindi.

Hii ni baada ya msako mkali kufanyika katika vitongoji vyote vya eneo la Kijiwe Tanga baada ya kumgonga mhudumu mmoja wa pikipiki na kufariki papo hapo.

Akizungumza na Wanahabari, Afisa mkuu wa Polisi eneo la Malindi Matawa Muchangi amesema kuwa washukiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka pindi uchunguzi utakapokamilika.

Muchangi amewataka wananchi kukoma kuchukua sheria mikononi mwao pindi ajali ama mkasa wowote unapotokea, akionya kuwa hatua hiyo hupelekea kupotea kwa ushahidi.

Taarifa na Charo Banda.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.