Washukiwa 22 wa ulanguzi wa mihadarati wakamatwa Kisauni

May 10, 2018

Maafisa wa polisi katika eneo la Kisauni wamewatia nguvuni washukiwa 22 wa ulanguzi wa dawa za kulevya huku msako dhidi ya walanguzi ukiimarishwa katika eneo hilo.

Kamanda mkuu wa Polisi kaunti ya Mombasa Johnstone Ipara amesema eneo la Kisauni limeathirika zaidi na hali hiyo, akihoji kuwa Maafisa wa usalama wanaendeleza msako dhidi ya wahusika ili kuikabili hali hiyo.

Akizungumza mjini Mombasa, Ipara amesema msako huo utaendelezwa katika maeneo mengine ya kaunti hiyo ili kuwaokoa vijana wadogo ambao wameathirika na utumizi wa dawa za kulevya.

Hata hivyo, amekiri kuwa ulanguzi na utumizi wa dawa za kulevya katika kaunti hiyo umechangia kudidimia kwa hali ya usalama katika kaunti nzima ya Mombasa.

Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.