Washukiwa wa ulaghuzi wa mihadarati chuma chao kimotoni

June 25, 2018

Huku siku ya kimataifa ya matumizi ya mihadarati ikitarajiwa kuadhimishwa hapo kesho, Mshirikishi mkuu wa ukanda wa Pwani Benard Lempara Marai ameagiza kukamatwa na kushtakiwa kwa walanguzi wote wa dawa ya kulevya.

Akitoa agizo hilo mjini Kilifi katika kikao cha vijana kilichoandaliwa na Shirika la NACADA, Lempara amesema muda mrefu maafisa wa usalama wamekuwa wakihongwa na walanguzi hao ili kuendeleza biashara zao zinazowadhuru wananchi.

Asema amesema mali zote za walanguzi wa dawa za kulevya watakaopatikana zitarudishwa kwa serikali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirika la NACADA, Julius Gathire amewataka wananchi kuwajibika katika kupiga vita mihadarati huku akiwataka waathiriwa wa mihadarati kujisajili katika makundi ili wafaidike na huduma za NACADA.

Taarifa na Marieta Anzazi.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.