Washukiwa wa uwindaji haramu Kwale wafikishwa mahakamani

December 18, 2017

Washukiwa wawili wa uwindaji haramu wamefikishwa katika mahakama ya Kwale kujibu shtaka la kupatikana na pembe za ndovu kinyume cha sheria.

Mshukiwa wa kwanza Said Kuzidi Mwachitema mnamo tarehe 15/ 12/2017 katika kijiji cha Mtsangatamu huko Matuga kaunti ya Kwale alipatikana na pembe 2 za ndovu zenye uzani wa kilo 34 zinazoaminika kuwa za thamani ya Shilingi milioni 3.4.

DSC09695 3

Naye mshukiwa wa pili Hasira Makotti Mwanzala mnamo tarehe 15 /12 /2017 katika kijiji cha Tiribe huko Matuga kaunti ya Kwale alipatikana na pembe mbili za ndovu zenye uzani wa kilo 16 zinazoaminika kuwa za thamani ya Shilingi milioni 1.6.

DSC09697 2

Mbele ya hakimu mkaazi Paul Mutai wawili hao wamekanusha mashtaka hayo na kuachiliwa kwa dhamana ambapo mshukiwa Saidi Kuzidi ameachiliwa  kwa dhamana ya Shilingi milioni 6 ama pesa taslim shilling milioni 3  huku mshukiwa Hasira Makotti Mwanzala akiachiliwa kwa dhamana ya Shilingi million 5 au pesa taslim Shilingi million 2. Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 2/1/2018 na kusikizwa tarehe 12/2/2018. Wawili hao wanazuiliwa rumande baada ya kushindwa kulipa dhamana hiyo.

Taarifa na Mariam Gao.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.