Wasiwasi watanda baada ya mifugo kuzuiliwa Magarini

April 30, 2018

Maafisa wa polisi kwa ushirikiano na wasimamizi wa shamba la ADC huko Magarini kaunti ya kilifi wanaizuilia mifugo ya wakaazi iliyopatikana ikilisha katika shamba hilo kinyume cha sheria.

Kulingana na msimamizi wa shamba hilo Murasi Murupi wakulima wa eneo hilo wamevamia shamba hilo na kuendeleza shughuli za kilimo sawa na kuiuwa mifugo inayomilikiwa na usimamizi wa shamba hilo punde inapoharibu mimea yao.

Murupi vile vile amesema kuwa kufikia sasa takriban asilimia 90 ya ardhi ya shamba hilo la ADC imevamiwa na wakuliwa kutoka maeneo ya Kijiwetanga, Matsangoni na Watamu.

Wakati uo huo amedai kwamba kuna kamati ya matapeli inayochochea wakaazi wa eneo hilo kuvamia shamba hilo.

Taarifa na Esther Mwagandi.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.