Watu wawili wapigwa risasi Kwale

May 15, 2018

Picha/Kwa hisani

Watu wawili wanahofiwa kufariki baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana katika eneo la Matairini barabara kuu ya Kwale –Kombani asubuhi ya leo.

 Wawili hao mwendesha bodaboda na abiria wake waliokuwa wakielekea eneo la Kombani mwendo wa saa nne asubuhi inadaiwa walikuwa wametoka katika mahakama ya Kwale ambapo inasemekana abiria huyo alitoa ushahidi katika kesi.

Walioshuhudia tukio hilo wanasema kuwa wamepata  maganda ya risasi  katika eneo la tukio  licha ya kuwa  hapo awali  ilisemekana wawili hao waliangamia katika ajali ya barabarani.

Hata hivyo wanasema kuwa wameshangazwa na jinsi maafisa wa polisi walivyofika katika eneo la tukio na kuokota maganda ya risasi bila ya kufuata utaratibu wake. Hata hivyo hadi kufikia sasa idara ya usalama kaunti ya Kwale hawajazungumzia tukio hilo.

Taarifa na Radio Kaya.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.