Wavuvi Mombasa walalamikia mazingira duni

June 5, 2018

Wavuvi katika kaunti ya Mombasa wamelalamikia mazingira duni ya baharini yanayotoka na utupaji taka kiholela.

Wakiongozwa na Naibu Mwenyekiti wa Kitengo cha usimamizi wa fukwe za bahari mjini Mombasa Abdallah Mwandia, wavuvi hao wamesema tabia ya usafirishaji wa taka baharini umelemaza pakubwa shughuli za uvuvi.

Mwandia ameilaumu Wizara za Mazingira kwa kukosa kuwajibikia majukumu yake huku akihimiza kubuniwa mbinu mbadala za kukabiliana na swala hilo ili kuboresha mazingira ya bahari.

Kwa upande wake Waziri wa Mazingira kaunti ya Mombasa Godfery Nato amesema tayari serikali ya kaunti hiyo imesitisha utupaji taka kwenye sehemu zilizoko karibu na ufukwe wa bahari.

Taarifa na Hassein Mdune.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.