WAVUVI WAITAKA KPA KUKARABATI BOTI KABLA YA KUWAPA

June 6, 2018

Baadhi ya wavuvi kaunti ya Mombasa walioathirika na upanuzi wa bandari ya Mombasa, wamependekeza kufanyiwa marekebisho na kuongezwa uwezo boti wanazotarajiwa kupewa kama fidia.

Naibu katibu katika kitengo cha chama cha usimamizi wa fukwe za bahari Mombasa Wilson Rhumba amesema  boti husika zilikatiliwa awali na wavuvi baada ya kutofikia viwango vya kuweza kufanya shughuli za uvuvi katika maji makuu

Aidha Rhumba ameeleza kuwa wako tayari kuandamana na maafisa wa KPA hadi maji makuu kwa ukaguzi boti hizo na kukubali kuchukua boti zozote zitakazoweza kufanya shughuli za katika maji makuu.

Afisa katika kitengo cha sheria wa halmashauri ya bandari nchini KPA Wamuyu Ikegu amesema shirika hilo liko tayari kushirikiana kufanikisha swala hilo

Ikegu alikua akizungumza katika kongamano lililoleta pamoja wavuvi na maafisa wa halmashauri ya bandari nchini KPA, lililoandaliwa na Shirika la kijamii la Mombasa Port Civil Society Organization’ platform jijini Mombasa

Taarifa na Hussein Mdune

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.