WAWAKILISHI WA WADI KWALE WAMKEMEA MBUNGE

June 6, 2018

Baadhi ya wajumbe wa  bunge la kaunti ya Kwale wamemkea mbunge wa Msambweni Suleiman Dori, wakidai kuwa  alitoa matamshi ya kuidhalilisha  jamii moja katika kautni ya Kwale.

Wakiongozwa na  kiongozi wa walio wachache katika bunge hilo Ndoro Mweruphe,  wawakilishi hao  wamedai   Dori alimtaja mbunge wa Kinango Benjamin Dalu Tayari kama mtu pekee mweupe katika jamii yake, jambo wanalodai kuwa  ni kukosea heshima  watu wa jamii hiyo.

Kwa upande wake  mjumbe maalum katika bunge hilo Elizabeth Mangolo Ruwa   amesema kuwa matamshi ya Dori yalimdhalilisha  Tayari, huku akiongeza kuwa matamshi hayo yanawavunja moyo viongozi  chipukizi wanaoinuka  kwenye ulingo wa kisiasa.

Alipokuwa akimkaribisha Tayari  kutoa hotuba yake  wakati wa maadhimisho ya siku ya mazingira ulimwenguni  yalioongozwa na naibu rais William Ruto mjni Kwale, Dori alimtaja Benjamin Tayari kama mtu  pekee mweupe kwa jamii anayotoka.

Taarifa na Michael Otieno

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.