Wawakilishi wadi wamtaka Mvurya kuteua wasomi

February 11, 2019

SALIM MVURYA

Baadhi ya Wawakilishi wa wadi katika bunge la kaunti ya Kwale, Sasa wanamtaka Gavana wa kaunti hiyo Salim Mvurya, kuwateua viongozi waliohitimu kuongoza idara muhimu ili wananchi wapate huduma bora.

Mwakilishi wa wadi ya Kubo South kaunti ya Kwale Andrew Mulei, amesema baadhi ya miradi imedorora katika kaunti hiyo, kutokana na uteuzi wa viongozi wasiowajibikia majukumu yao.

Mulei ametaja idara za maji na miundo msingi kama idara zilizofanya vibaya katika awamu ya kwanza ya uongozi wa Gavana Mvurya.

Mulei ametoa wito kwa Gavana Mvurya kukoma kufanya uteuzi wa viongozi kwa misingi wa kikabila, kwenye uteuzi wa maafisa wakuu wa idara mbalimbali wanaotarajiwa kupigwa msasa na wajumbe wa bunge la kaunti hiyo watakapotoka mapumzikoni.

Taarifa na Michael Otieno.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.