Wazazi wahimizwa kuwa wangalifu na watoto msimu huu wa likizo

December 2, 2017

Afisa wa maswala ya kijinsia na haki za watoto katika shirika la Haki Afrika Bi Salma Hemedi amesema kuwa wazazi wanapaswa kuwa waangalifu zaidi msimu huu wa likizo ili kuwakinga watoto dhidi ya maovu katika jamii.

Akiongea mjini Mombasa Bi Hemedi amesema kuwa wazazi watakua wakwanza kulaumiwa endapo watoto watapotoka kimaadilia na kukosa kurudi shule mapema mwakani.

Salma aidha amesema kuwa ni sharti wazazi watekeleze majukumu yao kikamilifu na wala sio kuwapa uhuru kupita kiasi kwani huenda ikawa na athari kubwa katika maisha ya watoto hao.

[Mwenda tezi na omo…….]

Mwanarakati huyo wa maswala ya jinsia hapa Pwani amekariri kwamba japo eneo la Pwani linafahamika vyema kwa mandhari yake ya starehe, starehe hizo kamwe hazifai kuwafikia watoto.

Taarifa na Gabriel Mwaganjoni.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.