Wazazi walaumiwa kwa ongezeko la wanafunzi wanaokosa shule za upili

January 10, 2019

Mwalimu mkuu wa shule ya upili yaGolini, Changawa Shungu.

Naibu mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Golini, Changawa Shungu.

Naibu Mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Golini kaunti ya Kwale Shungu Changawa Madaraka, amesema ongezeko la idadi ya wanafunzi wanaokamilisha darasa la nane na kukosa kujiunga na shule za upili linachangiwa na wazazi.

Changawa amesema wazazi huwachanganya watoto wao kwa kuwazuia kuripoti katika shule walizochagua na kusababisha watoto hao kukata tamaa ya masomo.

Ametoa wito kwa wazazi kuwapa watoto wao fursa ya kujiunga na shule walizochagua, akisema shule za umma ziko tayari kuwapokea wanafunzi wote.

Taarifa na Michael Otieno.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.