Wazazi watelekeza watoto wanaofikishwa mahakamani Kwale

November 9, 2018

Hakimu mkaazi wa mahakama ya mjini Kwale Patrick Wambugu ameshangazwa na jinsi wazazi wa kaunti ya Kwale wanavyotelekeza watoto wao wanaofikishwa mahakamani baada ya kutiwa mbaroni kwa makosa mbali mbali.

Akiongea wakati wa vikao vya mahakama katika mahakama ya mjini Kwale Wambugu amesema kuwa wazazi wengi wamekosa kufuatilia kesi za watoto wao wanapofikishwa kotini na kuilazimu mahakama kuwatafuta kwa msaada wa maafisa wa polisi.

Wambugu amewataka wazazi kutekeleza jukumu lao la ulezi vyema akisema wasipochukulia malezi ya watoto wao vyema, visa vya watoto kujitosa katika vitendo vya uvunjaji sheria vitazidi kukithiri.

Hakimu huyo mkaazi wa mahakama ya mjini Kwale ameihimiza jamii kwa ujumla kuwa karibu na watoto msimu huu wa likizo ndefu na kuwapa mawaidha kuhusiana na madhara ya kujiingiza kwenye uhalifu.

Taarifa na Mariam Gao.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.