Wazee wa Wakirundi waomba kupokoea malipo ya uzeeni

June 5, 2018

DSC02421WARUNDI

Licha ya wazee waliohitimu umri wa miaka 70 na zaidi kunufaika na pesa kila mwezi  katika mpango wa  malipo ya wazee maarufu 70 plus, wazee wa jamii ya warundi wanaoishi humu nchini wanadai mradi huo ni ndoto kwao.

Mwenyekiti wa jamii hiyo Shadrack Kiza Barnaba, amesema kwamba ukosefu wa vitambulisho vya kitaifa miongoni mwa watu wa jamii hiyo, umewasababisha kukosa kunufaika na fedha hizo.

Barnaba amewalaumu baadhi ya maafisa tawala kwa kuwatenga wakati wa ugavi wa pesa hizo, badala ya kuwasaidia kupata vitambaulisho vya kitaifa.

Saidi Kaijanua pia ni mmoja wa wanajamii hiyo wanaoishi katika wadi ya Kinondo kaunti ya Kwale.

Taarifa na Michael Otieno.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.