Waziri aahidi kukamilisha ujenzi wa viwanja Kwale

November 22, 2017

Waziri wa michezo, jamii na Ukuzaji wa Talanta katika kaunti ya Kwale Mohammed Bungale amewaahidi wakaazi wa Kwale kuwa ujenzi wa Viwanja katika kaunti hiyo utakamilika.

Ujenzi huo ulianza miaka mitano iliyopita lakini imekwama kwa muda hali iliyozua sintofahamu miongoni mwa wananchi.

Kulingana na waziri huyo changamoto kutoka kwa wanakandarasi ni miongoni mwa sababu zilizopelekea ujenzi wa viwanja hivyo kuchukua muda mrefu.

Taarifa na Mariam Gao.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.