We have, we have not?! Susumila akiri kumzimia Nyota Ndogo

November 27, 2017

Kitabu kitakatifu kinasema kuwa mja hunena yale yaliyojaa moyoni mwake.

Iwapo mambo ya hivi karibuni ni yakuzingatiwa basi moyo wa Yusuf Kombo maarufu kama Susumila ulikuwa umejaa mpaka pomoni maanake leo ameamua kufichua siri ya moyoni mwake.

Kupitia mtandao wa kijamii Susumila amekiri kuwa amekolea na penzi kumwelekea Nyota Ndogo.

“Leo najiuliza why, kila mtu anatabia yake nzuri na mbaya ila nahisi nyota ningempata tungeishi mpaka leo, I LOVE YOU @nyota_ndogo,” ameandika Susumila.

Tizama ujumbe huo kwa ukamilifu hapa chini.

SUSUMILA NYOTA NDOGO

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.