World Vision yatoa msaada kwa shule ya msingi ya Lotima

May 11, 2018

Wanafunzi wa shule ya msingi ya Lotima mjini Taveta kaunti ya Taita Taveta wamepata afuaeni baada ya shirika la World Vision kuwapa msaada.

Hii ni baada ya kuathirika pakubwa na mafuriko yaliyosababisha wanafunzi zaidi ya 200 kutoendelea na masomo.

Kwa mujibu wa afisa mkuu wa shirika la World Vision tawi la Taveta, Evelyne Mwazala ,msaada huo utawawezesha wanafunzi kusalia shuleni hadi msimu wa mvua utakapokamilika kwani njia nyingi wanazotumia wanafunzi hao zimeathirika na mafuriko na ni hatari kwao. Msaada huo ni wa mikeka ya kulalia,taa za sola,chakula miongoni mwa misaada mingine itakayowafaa wananchi.

Kwa upande wake afisa mkuu wa elimu katika eneo bunge la Taveta Hassan Abdurahman ametoa mwito kwa viongozi na washikadau wote katika sekta ya elimu kutoa usaidizi kwa shule zilizoathirika na mafuriko.

Taarifa na Fatuma Rashid.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.