Ziro ataka wanasiasa pwani kuungwa mkono.

May 9, 2018

Mwakilishi wa wadi ya Garashi katika eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi Peter Ziro ameeleza haja ya wakazi wa eneo hilo kuhakikisha wanaunga mkono viongozi wao kwa lengo la kuwekeza zaidi katika miradi ya maendeleo.


Kwa mujibu wa Ziro, huu sio wakati wa viongozi kupiga siasa akiwakosoa baadhi ya viongozi wanaozungumzia kuhusu siasa ya mwaka wa 2022 akiwataka wahudumie wananchi kuambatana na agenda zao za kampeni.
Wakati uo huo, Ziro ameapa kuwekeza zaidi katika sekta ya Elimu, kilimo na michezo kwa vijana miongoni mwa masuala mengine mengi ili kuhakikisha jamii ya eneo hilo inasonga mbele kimaendeleo.

Taarifa na Esther Mwagandi

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.