Kiraga awashauri wanasiasa wa Kilifi kushirikiana

May 8, 2018

Mwito umetolewa kwa viongozi wa kisiasa katika eneo la Magarini kaunti ya Kilifi kuweka kando tofauti zao za kisiasa na badala yake washirikiane kuleta maendeleo.

Akizungumza katika kikao kilichowaleta pamoja wagombea wote wa kiti cha uwakilishi wa wadi ya Gongoni katika uchaguzi mkuu uliopita, mwakilishi wa wadi hiyo kwa sasa Albert Kiraga Hare amesema kuwaunganisha wagombea wote na wananchi kwa ujumla kutapunguza joto la kisiasa na kutoa mazingira bora kwa maendeleo.

Kiraga amewahakikishia wakazi wa eneo hilo kwamba yuko tayari kushirikiana na viongozi hao katika ajenda mbali mbali za maendeleo zinazolenga kumnufaisha mwananchi wa kawaida pasi kujali misingi ya vyama, kabila wala dini.

Taarifa na Esther Mwagandi.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.