Mama Dangote – Picha Kwa Hisani.
Bi. Sanura Kasimu almaarufu Mama Dangote ambaye ni mama mzazi wa supastaa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, amemsifia aliyekuwa mpenzi wa zamani wa mwanawe, Wema Sepetu.
Diamond na Wema Sepetu – Picha Kwa Hisani
Ingawa kumekuwa na tetesi kwamba Diamond anatoka kimapenzi na mwanamuziki Zuchu huku uvumi huo ukiwavutia wengi na kutaka kujua kama ni kweli wasanii hao wanachumbiana.
Diamond na Zuchu – Picha Kwa Hisani
Mama Dangote ameonekana kuwa na mtanzamo tofauti na siku Jumanne alipakia video kwenye ukurasa wake wa Instagram ambako aliionekana akiwa amevalia dera alilonunuliwa na Wema Sepetu.
Kulingana naye, vazi hilo alinunuliwa na Wema Sepetu siku ya kuadhimisha kuzaliwa kwake na inabaki kama kumbukizi maishani.
Mashabiki wa wasanii hao wamebaki njia panda wakishindwa kwa nini Mama Dangote anaonekana kuwa hazungumzii mahusiano ya mwanawe na Zuchu ilhali Mamake Zuchu, Khadija Kopa, alizungumza kuhusu habari hizo.
Leave a Reply