Tume ya maadili na kupambana na ufisadi nchini EACC imesema mwaka uliopita wa kifedha ilipokea ripoti elfu 4,183 zinazohusiana na ufisadi, idadi ambayo ni ya chini ikilinganishwa na ripoti elfu 5,252 zilizowasilishwa mwaka wa kifedha 2022/2023.
Tume ya EACC imesema kati ya ripoti hizo elfu 4,183 zilizowasilishwa, ripoti elfu 1,846 zinazoambatana na majukumu ya tume hiyo ziliidhinishwa kwa uchunguzi.
Tume hiyo imesema kati ya ripoti hizo zilizoidhinishwa kwa uchunguzi, asilimia 37 zilihusha masuala ya rushwa, asilimia 19 zikihusiana na ubadhirifu wa fedha za umma, asilimia 10 zikiwa za umiliki mali ya umma kwa njia ya ulaghai, na asilimia 13 zikiwa za ukiukaji wa maadili.
EACC aidha imeripoti kwamba, mwaka uliopita wa kifedha vile vile ilifanikiwa kurejesha shilingi bilioni 3.4 ambayo ni mali ya umma iliyokua imepotea kwa njia za ufisadi.
Story by Mimuh Mohamed



