Huku hoteli na mikahawa mbalimbali katika kaunti ya Mombasa zikiendeleza harakati za maadhimisho ya sikukuu ya krismasi usimamizi wa hoteli na mkahawa wa Masai katika gatuzi dogo la Nyali umeenzi matayarisho hayo kwa aina yake baada ya kualika takriban nyumba za mayatima 5 kutoka kaunti ya Mombasa kuzuru hoteli hiyo na kuenzi sherehe hizo.
Akizungumza baada ya kupokea watoto mayatima zaidi ya 50 kutoka nyumba ya mayatima ya Barnabas mkuu wa mauzo katika mkahawa huo Josphat Iha amesema usimamizi wa mkahawa huo umeamua kutekeleza hatua hiyo kwani jamii imekosa kutoa msaada kwa watoto hao hali inayochangia mno unyanyapaa kwao.
Kauli iliyoungwa mkono na afisa wa masuala ya uhusiano wa umma Bi.Stella Muthoni aliyesisitiza ushirikiano wa jamii katika kuangazia watoto hao.
Naye rafiki ya mmiliki wa mkahawa huo na mteja mkuu wa mkahawa huo Mike Ritter amepongeza hatua ya usimamizi wa hoteli hiyo kutekeleza warsha kama hiyo.
Story by Bakari Ali



