Rwanda Air imerudisha rasmi safari za ndege kutoka taifa la Rwanda hadi uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moi jijini Mombasa.

Sekta ya utalii nchini imepigwa jeki baada ya kampuni ya usafiri wa angani ya Rwanda Air kurudisha rasmi safari za ndege kutoka taifa la Rwanda hadi uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moi jijini Mombasa. Kupitia kwa barua rasmi kutoka kwa mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara na viwanda nchini KNCCI tawi la Mombasa Abud Jamal […]
Idara ya mahakama Kwale imetishia kufunga nyumba saba za watoto eneo la Lunga-lunga.

Idara ya mahakama katika kaunti ya Kwale imetishia kuzifunga nyumba saba za watoto zilizo katika eneo bunge la Lunga-lunga, baada ya kubainika kwamba taasisi hizo hazijasajiliwa, zina usimamizi duni na zinajihusisha na vitendo haramu ikiwemo ulanguzi wa watoto. Akizungumza katika eneo la Tsuini,Vanga huko Lunga-lunga jaji wa mahakama kuu ya ardhi na mazingira kaunti ya […]
Visa vya ulawiti vimeongezeka kaunti ya Kwale, mashirika ya kutetea haki za kibinadamu yameingilia kati.

Mashirika ya kijamii yakiongozwa na shirika la Samba Sports Youth Trust yameelezea hofu kufuatia ongezeko la visa vya ulawiti katika kaunti ya Kwale. Akizungumza na wanahabari katika eneo la Kinondo Mkurugenzi wa shirika hilo Mohammed Mwachausa amesema hali hiyo inachangia ukiukaji mkubwa wa haki za watoto. Kwa upande wake afisa wa tume ya kutetea haki za kibinadamu nchini KHRC Irene […]
Kenya imeungana na mataifa mengine kuadhimisha siku ya ukimwi duniani,wadau wa afya watoa takwimu za maambukizi mapya.

Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya ukwimwi duniani leo Disemba Mosi, shirika la afya duniani WHO limesema kumaliza maambukizi ya HIV kufikia mwaka 2030, kunahitaji mikakati inayoangazia zaidi haki za kibinadamu, ushirikiano wa kimataifa, na uongozi wa kisiasa endelevu. WHO imesema licha ya mafanikio kushuhudiwa katika mapambano dhidi ya HIV kwa miongo kadhaa sasa, makabiliano hayo […]
Jaji mkuu nchini Martha Koome siku ya Jumatatu ameongoza hafla ya kuapishwa mhandisi Michael Kingi Thoya

Jaji mkuu nchini Martha Koome leo Jumatatu ameongoza hafla ya kuapishwa mhandisi Michael Kingi Thoya kuwa kamishna mpya wa tume ya kutathmini mishahara na marupurupu ya wafanyikazi wa umma SRC. Mhandisi Kingi atahudumu kwa muhula wa miaka sita na anachukua nafasi ya Dkt Anne Rwamba Gitau ambae muda wake wa kuhudumu ulikamilika tarehe 30 mwezi Juni mwaka huu. Kingi ameapishwa na […]