Harakati ambazo zimekuwa zikiendelezwa ili kuzima ukatili wa kijinsia mitandaoni zimeanza kuzaa matunda.

Harakati ambazo zimekuwa zikiendelezwa na wadau mbalimbali ili kuzima ukatili wa kijinsia mitandaoni zimeanza kuzaa matunda. Mratibu wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la Search for Common Ground linaloendeleza mchakato wa kuzikabili dhuluma za kijinsia mitandaoni humu nchini na haas katika Ukanda wa Pwani Hesbon Ndung’u amehoji kwamba mabadiliko hayo yamechangiwa na ushirikiano na jitihada za wadau mbalimbali […]
Jamii ya Huntha yaendelea kubaguliwa mashinani licha ya serikali kuitambua jinsia hiyo.
Licha ya Serikali kuitambua rasmi jinsia ya tatu humu nchini yaani watu waliyo na maumbile tata au Huntha, jamii hiyo imekuwa ikibaguliwa mashinani. Afisa kutoka Shirika linaloangazia haki za watu wasiyokuwa na jinsia moja rasmi yaani Huntha la Intersex Rights Initiative Coast-IRIC, Amina Ningala amesema ni vyema kwa jamii mashinani kuwakubali watu hao na kuwawezesha kujitambua kadri […]
Makundi ya watu wenye uatilifu kaunti ya Taita-taveta yahimizwa kutuma maombi ya zabuni.

Serikali ya kaunti ya Taita-taveta imesisitiza haja ya kushirikishwa watu wanaishi na ulemavu, kuboreshwa sera na kupanuliwa fursa kwa watu wanaoishi na ulemavu. Akizungumza katika kituo cha Kishushe, naibu gavana kaunti ya Taita taveta Christine Kilalo, amewataka wakaazi wa kaunti hiyo kuachana na tabia zilizopitwa na wakati za kuwatenga watu wanaoishi na ulemavu. Kilalo aidha […]
Stanley Kenga wa chama cha DCP atangaza azma ya kuwania tena nafasi ya ubunge katika uchaguzi wa mwaka 2027.

Siku chache tu baada Stanley Kenga wa chama cha DCP kushindwa kwenye uchaguzi mdogo wa ubunge wa Magarini kaunti ya Kilifi, kiongozi huyo sasa ametangaza azma ya kuwania tena nafasi hiyo katika uchaguzi wa mwaka 2027. Akizungumza katika eneo la Magarini Kenga amesema kwa sasa anaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha anapata uungwaji mkono katika uchaguzi […]
Chama cha UDA kimetoa ratiba ya uchaguzi wa mashinani wa chama hicho.

Chama cha UDA leo Disemba 4, kimefungua rasmi usajili wa wagombea wanaotaka kushiriki uchaguzi wa viongozi wa mashinani wa chama hicho. Bodi ya uchaguzi ya chama cha UDA kwenye taarifa yake leo Alhamisi, imesema usajili huo unaofanyika kwenye tovuti ya chama hicho, utakamilika rasmi tarehe 23 mwezi huu wa Disemba. Akitoa tangazo hilo mwenyekiti wa […]