Radiokaya

Friday, 13 February, 2026    4:05 pm

Play Listen Live

Serikali imeendeleza ukiukaji mkubwa wa haki za Wakenya bila kujali,wasema wanaharakati.

Licha ya watetezi wa haki za kibinadamu nchini kupigania haki na kuishinikiza Serikali kuheshimu haki za wananchi, Serikali imeendeleza ukiukaji mkubwa wa haki za Wakenya bila kujali. Afisa wa maswala ya dharura wa Shirika la kutetea haki za kibinadamu nchini la MUHURI Francis Auma amesema Kenya inashuhudia ukiukaji mkubwa mno wa haki za kibinadamu unaostahili juhudi za […]

Walimu wahimizwa kuchagua viongozi watakaosimama kidete kutetea maslahi ya

Mgombea wa nafasi ya naibu mwenyekiti wa chama wa walimu wa shule za upili na vyuo vya kadri nchini KUPPET tawi la kaunti ya Kwale Hamza Abdalla Musa, amewahimiza walimu kuchagua viongozi watakaosimama kidete kutetea maslahi yao, katika uchaguzi mkuu wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika Januari 2026. Akizungumza baada ya kuwasilisha stakabadhi zake katika afisi za KUPPET […]

Wakulima katika kaunti ya Taita taveta wameonywa dhidi ya kununua dawa za kuua wadudu kwa wachuuzi na maduka ambayo hayajaidhinishwa

Wakulima katika kaunti ya Taita taveta wameonywa dhidi ya kununua dawa za kuua wadudu kwa wachuuzi na maduka ambayo hayajaidhinishwa, wakati huu ambapo kunashuhudiwa ongezeko la uuzaji bidhaa gushi na zisizosalama. Haya yamesemwa na waziri wa kilimo katika serikali ya kaunti hiyo Dawson Katuu Mzenge, wakati serikali ya kaunti hiyo ikiendeleza kampeni ya kuhakikisha kilimo salama ndani […]

Naibu katibu mkuu wa chama cha UDA Daniel Ole Sambu ameaga dunia.

Naibu katibu mkuu wa chama cha UDA Daniel Ole Sambu, ameaga dunia siku ya Alhamisi. Akitoa tangazo hilo katibu mkuu wa chama cha UDA Hassan Omar Sarai amesema Ole Sambu alikua nguzo katika chama cha UDA na alikua nguvu kuu ya kuimarisha chama hicho mashinani. Sarai amesema Ole Sambu alikua na maono ya kimkakati, alijitolea kikamilifu kuimarisha […]

Wakenya kusherehekea sherehe za 62 za siku ya Jamhuri Disemba 12.

Wizara ya usalama wa ndani imetangaza mkakati wa kiusalama kabla ya sherehe za maadhimisho ya 62 ya siku ya Jamhuri zitakazofanyika kesho Ijumaa katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo. Mshirikishi wa utawala Gilbert Kitiyo amewataka wakenya wanaopanga kuhudhuria sherehe hizo, kuwa waangalifu na kuzingatia maagizo ya kiusalama yanayotolewa na mamlaka husika. Kitiyo amesema sherehe za mwaka huu […]