Radiokaya

Friday, 13 February, 2026    4:56 pm

Play Listen Live

Serikali imewaokoa wakenya 18 waliokua wamesajiliwa kushiriki vita kati ya Urusi na Ukraine.

Serikali ya kitaifa imefichua kwamba imefanikiwa kuwaokoa wakenya 18 waliokua wamesajiliwa katika vita vinavyoendelea kati ya Urusi na Ukraine. Kulingana na wizara ya masuala ya kigeni, wakenya hao wameokolewa baada ya kupiga simu wakiwa katika hali ya mfadhaiko, na tayari wamepewa nakala za dharura za kusafiri ili kurejea humu nchini. Mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi […]

Ajali za barabarani ugharimu Kenya asilimia 5 ya pato la taifa, yasema wizara ya uchukuzi

Waziri wa uchukuzi nchini Davis Chirchir ameeleza hofu kuhusu mzigo wa kiuchumi unaotokana na ajali za barabarani, akisema kila mwaka ajali za barabarani ugharimu Kenya ya asilimia tano ya pato lake la taifa. Kulingana na Chirchir Kenya hupoteza shilingi bilioni 800 kila mwaka kutokana na ajali za barabarani, na kiwango hicho ni gharama kubwa kwa […]

Bashatir awakosoa vikali wanaolenga kukigawanya chama cha UDA Mombasa

Mgombea wa kiti cha ubunge wa Kisauni kupitia kwa chama cha UDA katika kaunti ya Mombasa Mbarak Said Bashatir amewakosoa vikali baadhi ya viongozi wa chama hicho katika kaunti hiyo kwa kutaka kuleta mfurukano na mgawanyiko kati ya wanachama wa chama hicho katika kaunti ya Mombasa. Akizungumza kwenye mahojiano ya moja kwa moja na mwanahabari […]