Monday, 19January, 2026    8:44 am

Play Listen Live

Ajali za barabarani ugharimu Kenya asilimia 5 ya pato la taifa, yasema wizara ya uchukuzi

Waziri wa uchukuzi nchini Davis Chirchir ameeleza hofu kuhusu mzigo wa kiuchumi unaotokana na ajali za barabarani, akisema kila mwaka ajali za barabarani ugharimu Kenya ya asilimia tano ya pato lake la taifa.

Kulingana na Chirchir Kenya hupoteza shilingi bilioni 800 kila mwaka kutokana na ajali za barabarani, na kiwango hicho ni gharama kubwa kwa uchumi wa taifa.

Chirchir amesema serikali inafanYa kazi kwa karibu na mamlaka ya uchukuzi na usalama wa barabarani NTSA, kuendeleza kampeni kuhusu usalama wa barabarani ili kuzuia ajali za mara kwa mara.

Chirchir amewataka madereva kuwa waangalifu wanapokua barabarani akisema hatua ya madereva kuingia barabarani wakiwa walevi, wakiwa wamechoka au kuendesha gari kwa kasi ni kati ya tabia zinazochangia ajali hasa nyakati za usiku.

Story by Mimuh Mohamed

Contact Details

Radio Kaya

P.O Box 172~80403
Kwale, Kenya

SMS  – 0702 885 885

General Enquiries
info@radiokaya.co.ke

© 2025 Radio Kaya. All rights reserved.