Ashangazwa na kuwepo kwa socialites Mombasa

April 10, 2017

Na Dominick Mwambui

Kuinukia kwa wanasocialite katika mji wa Mombasa kumechukuliwa kama jambo la kawaida na wengi. Huku wengine wakisema kuwa mji huo unaenda na usasa.

Lakini mambo ni tofauti kwa msanii Katoi Wa Tabaka.

Msanii huyo ameshangazwa na habari kuwa mjini Mombasa kunao Socialites.

“Ati Mombasa kuna socialites? Basi Mombasa imeendelea maanake jinsi ninavyofahamu socialites sio watu wa chini katika jamii. Bado siamini kuwa Mombasa Kuna socialites,” amesema Katoi katika mazungumo maalum na Uhondo.

Kwa upande wako unadhani kuwa wanaojiita socialites mjini Mombasa wanafaa hadhi hiyo?

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.