Bamburi Cement, wametia saini mkataba wa uhandisi, ununuzi, na ujenzi wa shilingi bilioni 32 na kampuni ya Sinoma kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha klinka Matuga

Vijana katika eneo bunge la Matuga kaunti ya Kwale watanufaika na ajira kuanzia mwaka ujao. Hii ni baada ya Mtengenezaji mkuu wa bidhaa za saruji na zege nchini Kenya, Bamburi Cement, kutia saini mkataba wa Uhandisi, Ununuzi, na Ujenzi wa shilingi bilioni 32 na kampuni ya Sinoma kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha klinka […]
Kenya inatarajiwa kupata mvua nyingi na tofauti kubwa za halijoto kati ya Desemba 16 na Desemba 22

Kenya inatarajiwa kupata mvua nyingi na tofauti kubwa za halijoto kati ya Desemba 16 na Desemba 22, kulingana na utabiri wa hali ya hewa wa siku saba uliotolewa na Idara ya Hali ya Hewa ya Kenya (KMD). Katika ushauri wake, idara ilisema mvua inatarajiwa katika maeneo kadhaa, ikiwa ni pamoja na Nyanda za Juu Mashariki […]
Zaidi ya vijana 80 wadi ya Mjambere wanufaika na masomo ya kiufundi.

Zaidi ya vijana 80 kutoka wadi ya Mjambere gatuzi dogo la Kisauni wamenufaika na masomo ya kusuka, urembo,vipodozi na mapambo kutoka kwa wakfu wa Amriyah Juma Boy kama njia moja wapo ya kujiendeleza kiujuzi na kimaisha. Akizungumza kwenye hafla ya kufuzu kwa wanafunzi hao mdhamini mkuu wa masomo hayo wakili Amriyah Boy ambaye pia ni […]
Kampuni ya saruji ya Mombasa Cement imeanzisha rasmi shughuli zake za kila mwaka za kuboresha hadhi ya jiji la Mombasa msimu huu wa sherehe

Kampuni ya saruji ya Mombasa Cement imeanzisha rasmi shughuli zake za kila mwaka za kuboresha hadhi ya jiji la Mombasa msimu huu wa sherehe za krismasi na mwaka mpya mtawalia. Akizungumza kwenye barabara ya mzunguko ya Makupa gatuzi dogo la Mvita msimamizi mkuu wa mradi huo Gullam Mustapha Salim amesema hatua hiyo ni njia moja […]
Rais William Ruto kuongoza kikao cha baraza la mawaziri siku ya Jumatatu.

Rais William Ruto ameweka wazi kwamba safari ya kubadilisha taifa la Kenya kuwa taifa lililoendelea itaanza rasmi siku ya Jumatatu wakati wa kikao cha baraza la mawaziri. Akizungumza huko Gatundu kaunti ya Kiambu, rais Ruto amesema wakati wa kikao hicho baraza la mawaziri litaidhinisha hazina maalum ya miundo mbinu itakayohakikisha serikali inakusanya shilingi trilioni 5 […]
Serikali imeendeleza ukiukaji mkubwa wa haki za Wakenya bila kujali,wasema wanaharakati.

Licha ya watetezi wa haki za kibinadamu nchini kupigania haki na kuishinikiza Serikali kuheshimu haki za wananchi, Serikali imeendeleza ukiukaji mkubwa wa haki za Wakenya bila kujali. Afisa wa maswala ya dharura wa Shirika la kutetea haki za kibinadamu nchini la MUHURI Francis Auma amesema Kenya inashuhudia ukiukaji mkubwa mno wa haki za kibinadamu unaostahili juhudi za […]
Walimu wahimizwa kuchagua viongozi watakaosimama kidete kutetea maslahi ya

Mgombea wa nafasi ya naibu mwenyekiti wa chama wa walimu wa shule za upili na vyuo vya kadri nchini KUPPET tawi la kaunti ya Kwale Hamza Abdalla Musa, amewahimiza walimu kuchagua viongozi watakaosimama kidete kutetea maslahi yao, katika uchaguzi mkuu wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika Januari 2026. Akizungumza baada ya kuwasilisha stakabadhi zake katika afisi za KUPPET […]
Wakulima katika kaunti ya Taita taveta wameonywa dhidi ya kununua dawa za kuua wadudu kwa wachuuzi na maduka ambayo hayajaidhinishwa

Wakulima katika kaunti ya Taita taveta wameonywa dhidi ya kununua dawa za kuua wadudu kwa wachuuzi na maduka ambayo hayajaidhinishwa, wakati huu ambapo kunashuhudiwa ongezeko la uuzaji bidhaa gushi na zisizosalama. Haya yamesemwa na waziri wa kilimo katika serikali ya kaunti hiyo Dawson Katuu Mzenge, wakati serikali ya kaunti hiyo ikiendeleza kampeni ya kuhakikisha kilimo salama ndani […]
Naibu katibu mkuu wa chama cha UDA Daniel Ole Sambu ameaga dunia.

Naibu katibu mkuu wa chama cha UDA Daniel Ole Sambu, ameaga dunia siku ya Alhamisi. Akitoa tangazo hilo katibu mkuu wa chama cha UDA Hassan Omar Sarai amesema Ole Sambu alikua nguzo katika chama cha UDA na alikua nguvu kuu ya kuimarisha chama hicho mashinani. Sarai amesema Ole Sambu alikua na maono ya kimkakati, alijitolea kikamilifu kuimarisha […]
Wakenya kusherehekea sherehe za 62 za siku ya Jamhuri Disemba 12.

Wizara ya usalama wa ndani imetangaza mkakati wa kiusalama kabla ya sherehe za maadhimisho ya 62 ya siku ya Jamhuri zitakazofanyika kesho Ijumaa katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo. Mshirikishi wa utawala Gilbert Kitiyo amewataka wakenya wanaopanga kuhudhuria sherehe hizo, kuwa waangalifu na kuzingatia maagizo ya kiusalama yanayotolewa na mamlaka husika. Kitiyo amesema sherehe za mwaka huu […]