Monday, 19January, 2026    7:39 am

Play Listen Live

Bamburi Cement, wametia saini  mkataba wa uhandisi, ununuzi, na ujenzi  wa shilingi  bilioni 32 na kampuni ya Sinoma kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha klinka  Matuga

Vijana katika eneo bunge la Matuga kaunti ya Kwale watanufaika na ajira kuanzia mwaka ujao. Hii ni baada ya Mtengenezaji mkuu wa bidhaa za saruji na zege nchini Kenya, Bamburi Cement, kutia saini  mkataba wa Uhandisi, Ununuzi, na Ujenzi  wa shilingi  bilioni 32 na kampuni ya Sinoma kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha klinka katika  Matuga, Kaunti ya Kwale. Mbunge wa Matuga Kassim Tandaza amesema takriban vijana elfu 20 watanufaika na ajira.

Ujenzi wa kiwanda kipya cha klinka cha kisasa cha tani milioni 1.6 kwa mwaka, kinachojumuisha teknolojia za hali ya juu zisizo na kaboni ili kupunguza athari za mazingira, ni sehemu ya mkakati wa kampuni wa wa kuongeza mara mbili uwezo wake wa uzalishaji wa bidhaa bora za saruji na zege, ili kuwezesha maendeleo ya miundombinu ya Kenya na mabadiliko ya kiuchumi

Story by Correspondent

Contact Details

Radio Kaya

P.O Box 172~80403
Kwale, Kenya

SMS  – 0702 885 885

General Enquiries
info@radiokaya.co.ke

© 2025 Radio Kaya. All rights reserved.