Monday, 19January, 2026    8:17 am

Play Listen Live

Baraza la Mawaziri limeidhinisha Sera ya Kitaifa kuhusu Jamii za Wachache za Kikabila, Asili na Zilizotengwa

Rais William Ruto ametangaza kwamba Baraza la Mawaziri limeidhinisha Sera ya Kitaifa kuhusu Jamii za Wachache za Kikabila, Asili na Zilizotengwa. Rais aliielezea kama hatua kubwa kuelekea kutimiza ulinzi wa kikatiba kwa makundi yaliyo hatarini. Akizungumza wakati wa Siku ya Kimataifa ya Haki za Wachache Alhamisi, Rais Ruto alisema sera hiyo inatoa ramani kamili ya utekelezaji kamili wa Kifungu cha 56 cha Katiba, ambacho kinahakikisha hatua za upendeleo kwa jamii za wachache na zilizotengwa. Alibainisha kuwa sera hiyo ni matokeo ya mashauriano mapana ya kitaifa yanayohusisha jamii zilizoathiriwa, mashirika ya kiraia, serikali za kaunti, na wataalamu wa kiufundi.

Leo Alhamisi, rais  aliwakaribisha wajumbe 5,000 kutoka kwa makundi yaliyotengwa na ya wachache katika tukio la kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Haki za Wachache. Miongoni mwa jamii zilizowakilishwa ni Wandorobo, Ogiek, Dasenach, Njemps, Walwana, Rendille, Burji, El Molo, Sakuye, Suba, Kuria, Makonde, Shona, wanubi, miongoni mwa zingine.

 

Story by Jilani Mbura

Contact Details

Radio Kaya

P.O Box 172~80403
Kwale, Kenya

SMS  – 0702 885 885

General Enquiries
info@radiokaya.co.ke

© 2025 Radio Kaya. All rights reserved.