Mgombea wa kiti cha ubunge wa Kisauni kupitia kwa chama cha UDA katika kaunti ya Mombasa Mbarak Said Bashatir amewakosoa vikali baadhi ya viongozi wa chama hicho katika kaunti hiyo kwa kutaka kuleta mfurukano na mgawanyiko kati ya wanachama wa chama hicho katika kaunti ya Mombasa.
Akizungumza kwenye mahojiano ya moja kwa moja na mwanahabari wetu baada ya kutangaza rasmi azma yake hiyo kujitosa kinyang’anyironi kupitia kwa chama hicho Bashatir amesema ni sharti kwa viongozi kushirikiana na kuhakikisha wanaangazia maslahi ya mkaazi wa kaunti hiyo.
Kiongozi huyo aidha amepinga vikali kauli za baadhi ya wanachama na viongozi katika kaunti hiyo kudai kwamba chama hicho kina upendeleo wa baadhi ya viongozi bali kinazingatia sheria na muongozo wa kanuni za chama hicho.
Mwanasiasa huyo vilevile amesema kama viongozi wa chama hicho wanalenga kuleta umoja na uwiano kati ya viongozi na wanachama wa chama hicho ili kukimarisha chama hicho kote nchini.
Story by Bakari Ali Bakari



