Monday, 19January, 2026    8:31 am

Play Listen Live

Harakati ambazo zimekuwa zikiendelezwa ili kuzima ukatili wa kijinsia mitandaoni zimeanza kuzaa matunda.

Harakati ambazo zimekuwa zikiendelezwa na wadau mbalimbali ili kuzima ukatili wa kijinsia mitandaoni zimeanza kuzaa matunda.

Mratibu wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la Search for Common Ground linaloendeleza mchakato wa kuzikabili dhuluma za kijinsia mitandaoni humu nchini na haas katika Ukanda wa Pwani Hesbon Ndung’u amehoji kwamba mabadiliko hayo yamechangiwa na ushirikiano na jitihada za wadau mbalimbali kushiriki vita hivyo hasa baada ya kubainika kwamba kupanuka kwa matumizi ya utandawazi nchini kumekuja na fursa mbalimbali sawa na madhila yake.

Akizungumza katika Kaunti ya Mombasa wakati mchakato wa kudhibiti dhuluma za kijinsia ndani ya siku 16 za uanaharakati ukishika kasi, Ndung’u hata hivyo amehoji kwamba juhudi hizo zimewapatia kipau mbele vijana sawa na waundaji maudhui mitandaoni aliyowataja kama kiungo muhimu katika vita hivyo.

Kauli sawa na hiyo imetolewa na Mkereketwa wa maswala ya vijana ambaye pia ni Mwanafunzi wa chuo kikuu cha TUM Franklin Kimutai Lang’at aliyewahimiza vijana na hususan watumizi wa mitandao kukomesha ukatili wa kijinsia mitandaoni, akisema ukatili huo una athari za moja kwa moja kwa watumizi wa mitandaoni wanaopitia madhila hayo.

Hamasa hizo za kupambana na ukatili wa kijinsia mitandaoni zimeimarishwa nyanjani, jamii ikihimizwa kutosalia kimya au kupuuza dhuluma hizo na badala yake kuwaripoti wahalifu wanaoendeleza uovu huo mitandaoni ili waadhibiwe kisheria.

 

Story by Gabriel Mwambeyu

Contact Details

Radio Kaya

P.O Box 172~80403
Kwale, Kenya

SMS  – 0702 885 885

General Enquiries
info@radiokaya.co.ke

© 2025 Radio Kaya. All rights reserved.