Idadi ndogo ya vijana yajitokeza kwa zoezi la usajili wa makurutu

May 18, 2017

Na Lucy Makau

Kinango, KENYA, May 18- Idadi ndogo ya vijana imejitokeza  katika zoezi  la kusajiliwa makurutu wa  wanajeshi katika shule ya upili ya wavulana ya Kinango eneo la Kinango.

Luteni kanali  Cheruyot David amedokeza kuwa usajili wa makurutu hao ulianza mda ufao huku wakipeana muda wa saa moja na nusu kwa wale waliochelewa kutokana na changamoto ya kiusafiri ikizingatiwa baadhi ya barabara katika eneo hilo hazipitiki.

Luteni kanali  Cheruyot   ametoa mwito kwa wazazi wa eneo hilo kuzingatia masomo ya watoto wao haswa masomo ya hesabu, kingereza  na sayansi. Makurutu wengu walikua na alama nzuri  lakini wakaanguka upande wa masomo.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.