Monday, 19January, 2026    9:15 am

Play Listen Live

Idara ya usalama yaidhinisha mtaala mpya wa mafunzo ya polisi.

Inspekta jenerali wa polisi nchini Douglas Kanja amesema idara ya polisi nchini imebuni mtaala mpya wa mafunzo, ili kuwapa maafisa wa polisi ujuzi unaofaa kukabiliana na mahitaji yanayobadilika ya utekelezaji sheria.

Akizungumza katika chuo cha kitaifa cha polisi cha Kiganjo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya mwaka 2025 kwa askari wapya, Kanja amesema mtaala huo mpya unaangazia mazingira ya usalama yanayobadilika kufuatia mabadiliko ya teknolojia.

Kanja amesema mazingira ambayo maafisa wa polisi wanafanyia kazi kwa sasa ni yenye misukosuko, yasiotabirika na yenye changomoto, hivyo mtaala wa sasa utaangazia changamoto hizi.

Kanja amewataka makurutu watakaopata mafunzo hayo katika kipindi cha miezi tisa, kuzingatia nidhamu, na uzalendo.

Story by Mimuh Mohamed

Contact Details

Radio Kaya

P.O Box 172~80403
Kwale, Kenya

SMS  – 0702 885 885

General Enquiries
info@radiokaya.co.ke

© 2025 Radio Kaya. All rights reserved.