Tuesday, 16December, 2025    7:11 pm

Play Listen Live

Jaji mkuu nchini Martha Koome siku ya Jumatatu ameongoza hafla ya kuapishwa mhandisi Michael Kingi Thoya

Jaji mkuu nchini Martha Koome leo Jumatatu ameongoza hafla ya kuapishwa mhandisi Michael Kingi Thoya kuwa kamishna mpya wa tume ya kutathmini mishahara na marupurupu ya wafanyikazi wa umma SRC.

Mhandisi Kingi atahudumu kwa muhula wa miaka sita na anachukua nafasi ya Dkt Anne Rwamba Gitau ambae muda wake wa kuhudumu ulikamilika tarehe 30 mwezi Juni mwaka huu.

Kingi ameapishwa na msajili katika ofisi ya msajili mkuu Esther Nyaiyaki, ambapo Koome amemtaka Kingi kutambua kwamba wadhfa huo unakuja na jukumu la kuimarisha kifungu cha 230 cha katiba ya nchi kwa kuhakikisha mzigo wa mshahara unalingana na uwezo wa kifedha wa serikali.

Koome ameshikilia kwamba tume ya SRC ni taasisi ya kuimarisha uongozi, hivyo kamishna huyo mpya anapaswa kuhakikisha uhuru, uwazi, usawa na uwajibikaji katika kufanikisha majukumu ya tume hiyo.

 

Story by Mimuh Mohamed

Contact Details

Radio Kaya

P.O Box 172~80403
Kwale, Kenya

SMS  – 0702 885 885

General Enquiries
info@radiokaya.co.ke

© 2025 Radio Kaya. All rights reserved.