Monday, 19January, 2026    9:28 am

Play Listen Live

Kamati ya bunge yashutumu wanajeshi wa Uingereza wanaoendeleza mafunzo humu nchini kwa unyanyasaji.

Kamati ya bunge kuhusu ulinzi, ujasusi na uhusiano wa kigeni, imeshutumu wanajeshi wa uingereza walioko kwenye mafunzo humu nchini Kenya chini ya kitengo cha BATUK, kwa kutekeleza unyanyasaji wa kingono, ukiukaji wa haki za kibinadamu na uharibifu wa mazingira.

Kamati hiyo kwenye ripoti yake ya uchunguzi yenye kurasa 94, imeorodhosha ushuhuda wa kina kutoka kwa jamii katika kaunti za Laikipia na Samburu zilizokaribu na kambi hizo mafunzo, ambapo raia, wahanga, viongozi wa kijamii, mashirika ya kijamii na vitengo vya umma waliwasilisha ushahidi kwa kamati hiyo.

Ripoti hiyo imefichua kwamba jamii zilizo karibu na kambi hizo, zimelalamika kwamba wanajeshi wa kitengo cha mafunzo ya jeshi la Uingereza BATUK, wanatekeleza mauaji, kupigana hadharani, vifo vinavyotokana na matukio ya trafiki, utata katika uajiri na leba.

Madai dhidi ya wanajeshi hao yanayojulikana zaidi ni kuhusiana na mauaji ya Agnes Wanjiru mwenye umri wa miaka 21 mnamo mwaka 12 karibu na kambi ya mafunzo ya wanajeshi wa Uingereza katika mji wa Nanyuki, mshukiwa aliye mwanajeshi wa Uingereza Robert Purkiss, alikamatwa nchini Uingereza mwezi uliopita baada ya juhudi za miaka mingi za familia ya Wanjiru na mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini.

Hata hivyo, msemaji wa wizara ya ulinzi ya Uingereza amesema wizara hiyo inajutia sana changamoto ambazo zimejitokeza kuhusiana na uwepo wa walinzi wa Uingereza humu nchini Kenya, kwamba ziara hiyo iko tayari kuchunguza madai mapya katika ripoti hiyo punde ushahidi utakapotolewa.

 

Story by Mimuh Mohamed

Contact Details

Radio Kaya

P.O Box 172~80403
Kwale, Kenya

SMS  – 0702 885 885

General Enquiries
info@radiokaya.co.ke

© 2025 Radio Kaya. All rights reserved.