Monday, 19January, 2026    7:41 am

Play Listen Live

Kampuni ya saruji ya Mombasa Cement imeanzisha rasmi shughuli zake za kila mwaka za kuboresha hadhi ya jiji la Mombasa msimu huu wa sherehe

Kampuni ya saruji ya Mombasa Cement imeanzisha rasmi shughuli zake za kila mwaka za kuboresha hadhi ya jiji la Mombasa msimu huu wa sherehe za krismasi na mwaka mpya mtawalia.
Akizungumza kwenye barabara ya mzunguko ya Makupa gatuzi dogo la Mvita msimamizi mkuu wa mradi huo Gullam Mustapha Salim amesema hatua hiyo ni njia moja wapo ya kuadhimisha sherehe hizo sawia na ukuzaji utalii katika kaunti ya Mombasa.

Gullam aidha amesema kama usimamizi wa kampuni hiyo unalenga kuwendeleza miradi hiyo kama ilivyokuwa ikitekelezwa wakati wa utawala wa mmiliki wa kampuni hiyo Hasubhai Kanji Patel aliyeaga dunia mnamo Agosti 29,2024.Wakati uo huo, Gullam amesema kama usimamizi wa kampuni hiyo utashirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha wanaangazia changamoto mbalimbali zinazokumba jamii katika kaunti hiyo na Pwani kwa jumla.

Story by Bakari Ali Bakari

Contact Details

Radio Kaya

P.O Box 172~80403
Kwale, Kenya

SMS  – 0702 885 885

General Enquiries
info@radiokaya.co.ke

© 2025 Radio Kaya. All rights reserved.