Katibu atupilia mbali madai kuwa wamelitenga eneo la Rabai kimaendeleo

April 7, 2017

Na: Mercy Tumaini

Rabai, KENYA, Aprili 7 – Katibu  katika  wizara ya afya kaunti ya Kilifi Timothy Malingi amepuuza madai kuwa eneo la Jimba kaunti ya Kilifi limetengwa kimaendeleo na serekali hiyo ya kaunti.

Akiongea na wakaazi katika eneo la Mtandikeni  baada ya kuzindua rasmi ujenzi wa kituo cha afya katika eneo hilo, Malingi amesema kuwa wakaazi  eneo hilo  wamekosa kushirikiana na serikali ya kaunti wanapohitajika kutoa ardhi za kuendeleza miradi mbali mbali hali inayolazimu miradi hiyo kupelekwa kwengine.

Serikali ya kaunti ya Kilifi ilipanga kujenga zahanati katika eneo la Jimba lakini ikalazimika kupeleka mradi huo eneo la Mikomani.

Katibu  huyo wa wizara ya afya Kilifi ameahidi kwamba ujenzi wa kituo cha afya utakapokamilika, kitakuwa na madaktari na  wahudumu wa kutosha pamoja na madawa ya kutosha.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.