Story by Hussein Mdune-
Kama njia moja wapo ya kupiga jeki sekta ya utalii katika kaunti Kilifi na ukanda wa Pwani kwa ujumla, Shirika la maendeleo Pwani CDA limezindua rasmi hoteli na nyumba za wageni katika maeneo ya Mnarani kaunti ya Kilifi.
Akizungumza na Wanahabari baada ya uzinduzi huo, Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Mohammed Keinan amesema asilimia kubwa ya wakaazi hususan vijana hawana ajira na hoteli hiyo itazalisha viwango vya ajira kwa wakaazi wa eneo hilo.
Keinan amesema hoteli hiyo ambayo itakuwa ikipokea zaidi ya wageni 400 kwa siku imegharimu kima cha shilingi milioni 150, ambao ni ufadhili kutoka kwa benki kuu ya dunia
Hata hivyo ameweka wazi kwamba msimu huu wa sherehe za krismasi na mwaka mpya utaiwezesha hoteli hiyo kutumika na watalii mbalimbali ikiwemo wa kigeni na kinyumbani pamoja na kutumika kwa mikutano.