KINARA WA WIPER AHIDI KUONGEZA MGAO WA FEDHA NCHINI

April 10, 2017

Na: Michael Otieno

Kwale, KENYA, Aprili 10- Kinara wa chama cha Wiper, Stephen Kalonzo Musyoka ameahidi kuongeza mgao wa fedha wa serikali za kaunti kutoka asilimia 15 hadi asilimia 45  iwapo Muungano wa NASA utakapoingia uongozini.

Kalonzo amesema kuwa kaunti ya Kwale imebaki nyuma kimaendeleo kutokana na mgao mdogo wa fedha kutoka kwa serikali kuu kila mwaka.

Kiongozi huyo wa Wiper amewarai wakaazi wa kaunti ya Kwale kuupigia kura Muungano wa NASA kwenye uchaguzi mkuu ujao, sawia na kumchagua Balozi Mwakwere kuwa gavana wao wakati wa uchaguzi mkuu.

RADIO KAYA 93.1 FM (MSA), 99.7 FM (MLD) NA 94.9 VOI NA VIUNGA VYAKE.