Monday, 19January, 2026    7:57 am

Play Listen Live

Makundi ya watu wenye uatilifu kaunti ya Taita-taveta yahimizwa kutuma maombi ya zabuni.

Serikali ya kaunti ya Taita-taveta imesisitiza haja ya kushirikishwa watu wanaishi na ulemavu, kuboreshwa sera na kupanuliwa fursa kwa watu wanaoishi na ulemavu.

Akizungumza katika kituo cha Kishushe, naibu gavana kaunti ya Taita taveta Christine Kilalo, amewataka wakaazi wa kaunti hiyo kuachana na tabia zilizopitwa na wakati za kuwatenga watu wanaoishi na ulemavu.

Kilalo aidha amesema ni muhimu kwa watu wenye uatilifu kuelimishwa na kuhimizwa kujisajili ili kupata vitambulisho vitakavyowawezesha kujumuishwa kwenye miradi inayoidhinishwa na kaunti hiyo.

Kwa upande wake afisa wa afya kaunti hiyo Dkt Rukia Mkamburi amesema zaidi ya watu elfu moja wanaoishi na ulemavu wamefanyiwa ukaguzi katika kaunti hiyo na kukabidhiwa vyeti hitajika.

Naye mwakilishi wa baraza la kitaifa la watu wanaoishi na ulemavu katika kaunti hiyo Fatuma Kadzo ameeleza umuhimu wa watu wenye uatilifu kujisajili kupitia mfumo wa e-Citizen ili wapate vyeti na kunufaika na huduma za serikali ikiwemo kuondolewa mzigo wa ushuru.

Wakati uo huo afisa mkuu wa masuala ya vijana,michezo, jinsia na huduma za jamii katika kaunti hiyo Elizabeth Mbinga ameyataka makundi ya watu wenye uatilifu kutuma maombi ya zabuni.

 

Story by Mimuh Mohamed

Contact Details

Radio Kaya

P.O Box 172~80403
Kwale, Kenya

SMS  – 0702 885 885

General Enquiries
info@radiokaya.co.ke

© 2025 Radio Kaya. All rights reserved.